KIPA namba tatu wa Yanga Ramadhani kabwili ameondolewa kwenye kambi ya timu hiyo baada ya kupata taarifa za mama yake mzazi presha kushuka kabla ya kukimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Hiyo ikiwa ni siku moja tangu kipa huyo aitwe na maofisa wa Takukuru kwaajili ya kuhojiwa baada ya kudaiwa kutoa taarifa za kuahidiwa kupewa gari aina ya IST na mmoja wa viongozi wa Simba endapo angekubali kupewa kadi ya njano ili akose mchezo unaofuata waliotarajiwa kukutana na watani wao Simba
Post a Comment