IMEELEZWA kuwa majembe matatu ndani ya Yanga yamepewa kazi maalumu ya kumalizana na Coastal Union leo Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Nyota hao ni pamoja na kiungo raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima, Bernard Morisson raia wa Ghana na Ditram Nchimbi ambaye yeye ni mzawa.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa amesema kuwa kila mchezaji ndani ya kikosi cha Yanga amepewa majukumu yake jambo litakalorahisisha kazi yao mbele ye Coastal Union.

"Wachezaji wote tumewapa majukumu ya kufanya ikiwa ni pamoja na Niyonzima, Nchimbi na Morrison ili kuongeza nguvu ya ushindi.

"Kila mmoja ana kazi ya kushirikiana na wengine hilo lipo wazi na kwa sasa tumejipanga kufuta makosa ya mechi zetu zilizopita," amesema.

Yanga ikiwa imecheza mechi 21 imekusanya jumla ya pointi 40 imefunga mabao 25 na imefungwa mabao 18

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.