Serikal ya Jamhuri wa Tanzania kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kufuatilia kwa karibu malalamiko yote yanayotolewa na wadau wa soka mara kwa mara katika Ligi Kuu na ligi nyingine.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara hiyo iliyotolewa leo, Jumatano, Dk Mwakyembe ameliagiza Baraza hilo kutoa mrejesho wa agizo hilo ndani ya siku tatu.

“Wizara inaendelea kupokea tuhuma mbalimbali/uonevu katika mashindano ya Ligi mbalimbali za mpira wa miguu yanayoendelea nchini, lakini wdau hawaoni hatua zikichukuliwa mara moja na kupatiwa mrejesho,” taarifa hiyo imemnukuu Waziri huyo.

Wakati huo huo, Rais wa TFF, Wallace Karia ameiagiza Bodi ya Ligi kukutana na Kamati ya Waamuzi kutathmini mwenendo wa uchezeshaji wa soka nchini. Lengo la mkutano huo ni kuhakikisha malalamiko dhidi ya uchezeshaji yanafanyiwa kazi

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.