Beki mkongwe wa Yanga, Kelvin Yondani amesema kuwa anafahamu alipoteza namba katika kikosi cha kwanza katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu Bara na sasa amerudi upya huku akiwataka mashabiki wa timu hiyo kupata soka safi kutoka kwake.
Awali, beki huyo alikuwa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Mbelgiji Luc Eymael kwa kile kilichoelezwa kuonyesha nidhamu mbaya kwa kutoonekana mazoezini kwa siku tatu huku simu yake ikiwa imezimwa na baadaye kurejea kikosini na kuondolewa.
Beki huyo baadaye alirejeshwa kikosini, lakini hakuwa anapata nafasi ya kucheza huku nafasi yake ikichezwa na Juma Makapu, kabla ya juzi kurejea uwanjani katika mchezo wa ligi walipocheza na Mbeya City na kutoka sare ya 1-1.
Yondani alisema: “Nikwambie tu ili timu iwe bora lazima kila nafasi iwe na ushindani, hii ni funzo kwangu kuendelea kujituma na kuhakikisha napata nafasi yakucheza mara kwa mara kwani ndicho kilichonileta Yanga.
“Katika nafasi hii ninayocheza wachezaji wote waliokuwepo wana uwezo wa kucheza, kikubwa kinachotakiwa kwangu ni kutimiza majukumu nitakayopewa ya kuokoa na kupunguza hatari golini kwetu,” alisema Yondani
Post a Comment