MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa Kagere Sugar amesema kuwa wataendelea kutoa dozi ndani ya Uwanja wa Kaitaba ili kuongeza nafasi ya kufikia malengo ambayo wamejiwekea.
Mwadui FC ya Shinyanga iliambulia dozi ya mabao 2-1 kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Kaitaba, leo Biashara United itakutana na moto wa Kagera Sugar.
Akizungumza na Saleh Jembe, Maxime amesema kuwa malengo ya timu ni kupata pointi tatu kwenye mechi zao zote zilizobaki ili kulinda heshima ya timu yake.
“Ushindani ni mkubwa kwenye ligi nasi tunatakiwa kukomaa kupata ushindi, tukiwa nyumbani tunakuwa na mashabiki zetu ni muhimu kwetu kutoa dozi ambayo itatupa pointi tatu muhimu, mashabiki watupe sapoti,” amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.