JONAS Mkude, kiungo ndani ya Simba ameonyesha kitendo ambacho kimeniacha nikitafakari uimara wake na yale anayoyafanya ndani ya Uwanja kwa sasa.
Licha ya kwamba ubora wake unazidi kuimarika ila matendo yake kwa kiasi kikubwa yanarudisha nyuma thamani yake na kushusha ule ubora wake.
Mguuni ana mabao mawili aliyotupia kwa sasa msimu wa 2019/20 alianza mbele ya Alliance alipewa pasi na Sharaf Shiboub na kuibukia bao lake la pili mbele ya Mbao alipewa pasi na Ajibu pia yumo kwenye kutoa pasi za mwisho akiwa nazo tatu.
Wakati akitoa pasi yake ya tatu mbele ya Biashara United Uwanja wa Taifa bao lililofungwa na kiungo Luis Miquissone nilishuhudia tukio ambalo si la kiungwana ndani ya Uwanja hasa kwa mchezaji mkomavu Mkude.
Ilikuwa dakika ya 56 alimpa purukushani mchezaji wa Biashara United, Ally Kombo, jambo hili si la kiungwana kwani mlinzi wa mchezaji wa mpira ni mchezaji mwenyewe.
Kamera za Azam TV zilionyesha kwamba wakati wa harakati za kusepa na mpira, Mkude alimgonga kwa mikono (Kiwiko) mchezaji wa Biashara United Kombo jambo ambalo si la kiungwana.
Matukio haya yamekuwa yakijirudia kwa wachezaji wetu wengi ndani ya ligi na yakiendelea itakuwa ni hatari kwa afya ya soka letu.
Wakati lile la Bernard Morrison likitafutiwa ufumbuzi baada ya kumgonga kiwiko mchezaji wa Tanzania Prisons hili nalo linaibuka usisahau pia na Wawa naye aliwahi kufanya vitendo hivi.
Wachezaji wetu ni muhumu kulinda afya za wachezaji wenzenu hata ikiwa ni shughuli ya kutafuta ushindi nguvu kiasi ila usalama kwanza.
Mkude wewe ni jasiri na mkomavu kwenye ligi unapaswa uwe mfano kwa wale wanaokufuata unapaswa uwe muungwana ndani ya Uwanja, hasira na mabavu sio mchezo mzuri
Post a Comment