Mshambuliaji wa Yanga, Tariq Self Kiakala, amewaambia mashabiki wa timu hiyo kuwa yupo fiti na amepona kabisa majeraha yake.
Tariq aliumia mguu katika mchezo dhidi ya Biashara United uliochezwa mwishoni mwa mwaka jana katika Uwanja wa Taifa, Dar. Tangu hapo hajaonekana akicheza.
“Nashukuru Mungu nimepona majeraha yangu, niko fiti na nimeanza mazoezi na wachezaji wezangu kuhakikisha naendelea kuwa fiti katika kuitumikia timu yangu.
“Nitakuwa tayari kuisaidia timu yangu mwalimu akinipa nafasi, naamini kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele ndipo nitakapokuwa fiti zaidi,” alisema Tariq ambaye alijiunga na Yanga katika usajili wa dirisha dogo uliofungwa Januari 15, mwaka huu
Post a Comment