IMEELEZWA kuwa michuano mikubwa ya SportPesa Super Cup ipo njiani kurejea tena na safari hii ushindani ukitajwa kuwa mkubwa zaidi ya msimu ulipita.

Mdhamini mkuu wa michuano ya SportPesa Super Cup ni Kampuni ya kubashiri ya SportPesa ambayo imewekeza kwenye kuinua soko la mpira wa Tanzania na imedhamini timu kubwa ambazo ni pamoja na Simba, Yanga, Namungo.

Habari zinaeleza kuwa kwa sasa wadhamini hao wanasubiri kutoa tamko kuhusu uwepo wa michuano hiyo ambayo hutoa fursa kwa bingwa kucheza na timu ya Everton ya England ambayo nayo pia inadhaminiwa na kampuni hiyo.

Gormahia ni bingwa mara mbili wa kobe hilo na bingwa mtetezi ni Kariobargs Sharks aliyeshinda mbele ya Bandari kwenye fainali iliyochezwa Uwanja wa Taifa

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.