LICHA ya Ante Rebic wa AC Milan kufunga bao la kuongoza kwa timu yake dakika ya 40 na Zlatan Ibrahimovic kupachika msumari wa pili dakika ya 45 haikuwazuia AC Milan kupindua meza kibabe kipindi cha pili.

Mpaka muda wa mapumziko AC Milan walikuwa mbele kwa mabao mawili na yalidumu mpaka dakika ya 50 kipindi cha pili ambapo Inter Milan walizinduka.

Dakika ya 51 Marcelo Brozovic alipachika bao la kwanza na dakika ya 53 Matias Vecino aliweka mzani sawa na kufanya ngoma iwe 2-2.

Stefan de Vrij alipachika bao la tatu kwa Inter Milan kabla ya Romelu Lukaku kumaliza nguvu za wapinzani wao dakika ya 90+3 kwa kufunga bao la mwisho na kuwafanya washinde mabao 4-2.

Matokeo hayo yanaifanya Inter Milan kuwa nafasi ya kwanza ndani ya Seria A ikiwa na pointi 54 kwa tofauti ya mabao manne na Juventus ambao nao wana pointi 54 wakiwa nafasi ya pili.

AC Milan ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 32 kwenye Msimamo na zote zimecheza mechi 23

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.