IMEELEZWA kuwa Klabu ya Barcelona inaweza kufanya usajili maalumu msimu huu ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chake.
Kwa sasa kikosi hicho kina wachezaji wawili ambao ni majeruhi watakaokaa nje ya Uwanja muda mrefu.
Ousmane Dembele ameungana na mshambuliaji Luis Suarez kwenye orodha ya majeruhi jambo ambalo limevuruga hesabu ndani ya timu.
Licha ya dirisha la usajili kufungwa bado kanuni zinaruhusu kwa klabu kufanya hivyo endapo kutakuwa na majeruhi watakaovuruga hesabu za timu, ndivyo mambo yalivyo kwa sasa.
Upo uwezekano wa Barcelona kuomba kibali na inaweza kusajili mchezaji yoyote kutoka ndani ya Hispania au yeyote ambaye hana klabu.
Ikiwa mipango itajibu basi Christhian Stuan na William Sociedad wanapigiwa chapuo kuingia kwenye utawala wa Kocha Mkuu wa Barcelona, Quique Setien
Post a Comment