AZAM FC iliyo chini ya Kocha Mkuu Arstica Ciaoba raia wa Romania leo ina kibarua mbele ya Polisi Tanzania Uwanja wa Uhuru mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa majira ya saa 10:00.
Matajiri hao wa Dar watashuka uwanjani na kumbukumbu ya kushinda mabao 3-1 mbele ya KMC kwenye mchezo wa ligi kuu.
Idd Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa wanaiheshimu Polisi Tanzania wataifuata kwa tahadhari kubwa huku hesabu ikiwa ni pointi tatu.
"Tunawaheshimu wapinzani wetu ni timu imara na bora, tutaifuata kwa tahadhari ili kupata kile ambacho tunakihitaji ambacho ni pointi tatu," amesema.
Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 41 huku Polisi Tanzania ikiwa nafasi ya saba na pointi zake 30 zote zimecheza mechi 20

Post a Comment