February 2020

Mchezaji wa Aston Villa ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta, amethibitisha kuwa watu zaidi ya 10 kwenye familia yake, watakuwepo kwenye uwanja wa Wembley kutazama fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Man City.

Samatta ameweka wazi hilo kwenye mahojiano aliyofanya na The Gaurdian, ambapo amelieleza gazeti hilo pamoja na mtandao wao, kuwa ndugu zake hao watakuwa jukwaani.

'Zaidi ya wanafamilia/ndugu 10 wa Mbwana watakuwepo kwenye uwanja wa Wembley jijini London Uingereza, wakimtazama akicheza mechi ya fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Man City kesho Saa 1:30 Usiku', wameandika The Guardian.

Katika mahojiano hayo Samatta hajataja ni ndugu gani watakakuwepo London, kumtazama akiweka historia hiyo ya kucheza Wembley ambao ni uwanja wa taifa wa England.

Samatta amesajiliwa na Aston Villa kwenye dirisha dogo na tayari ameshafunga goli kwenye mechi yake ya kwanza kwenye Premier League ambayo ilikuwa dhidi ya Bournamouth.

RUVU Shooting jana, Februari 29, 2020 iliipapasa mabao 2-0 Mbao FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mabatini, Pwani.

Kwenye mchezo huo Ruvu Shooting ilimnyoosha bosi wao wa zamani aliyeinusuru timu kushuka daraja, Abdulmutik Hajji ambaye kwa sasa yupo Mbao FC.

Kwenye mchezo huo nyota wa Mbao FC Iganas Chuma alikimbizwa hspitali ya Mlandizi  kupata matibabu baada ya kuumia mguu.

LEO Mbwana Samatta, mshambuliaji anayekipiga timu ya Aston Villa atakuwa na kazi ya kukipiga mbele ya Manchester City kwenye mchezo wa Kombe la Carabao.

Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Wembeley na unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na asili ya fainali za kuwa ngumu kwa timu zote.

Samatta ataweka rekodi ya kukutana uso kwa uso na mastaa wa Manchester City ambao ni akina Aguero,Kocha Mkuu Pep Guardiola.

Villa ilitinga hatua ya fainali kwa ushindi wa mabao 3-2 baada ya mchezo wa kwanza kutoshana nguvu na Leicester kwa kufungana bao 1-1 na kwenye mchezo wa pili wa nusu fainali, Villa ilishinda mabao 2-1 na ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Samatta.


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umejipanga kuona unapata matokeo chanya kwenye mechi zake zote za Ligi Kuu Bara ikiwa ni pamoja na mchezo wa watani wao wa jadi Simba utakopigwa Machi 8 Uwanja wa Taifa.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa baada ya kumaliza gundu la sare sasa hesabu zao ni kuona wanashinda mbele ya Simba Machi 8.

"Tumewachapa Alliance licha ya manenomaneno, kwa sasa tupo tayari na hata mchezo wetu wa mwezi Machi tutawashinda wapinzani wetu, wape salaamu,".

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa Simba ikiwa mwenyeji ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2


ANDREW Simchimba, mshambuliaji wa Azam FC jana ameiokoa timu yake usiku kuweza kusepa na pointi tatu mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Bao hilo la ushindi lilifungwa dakika ya 90 na kuifanya JKT ipoteze matumaini ya kusepa na pointi moja kwenye mchezo huo ambao wao walikuwa wenyeji.

Azam FC inafikisha pointi 48 ikiwa imecheza mechi 25 inajikita nafasi ya pili huku kinara akiwa ni Simba mwenye pointi 62.


GEOFREY Luseke, beki wa timu ya Alliance amesema kuwa hawakustahili kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wapinzani wao Yanga.

Jana, Februari 29, Alliance ya Mwanza ilikubali kichapo kutoka kwa Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Luseke amesema:'Haikuwa mipango yetu kupoteza mbele ya wapinzani wetu Yanga ila kutokana na wao kutumia makosa yetu basi wameweza kutushinda kwa sasa tunajipanga kwa ajili ya mechi zinazokuja," .

Alliance FC ipo nafasi ya 13 imejikusanyia pointi 29 kibindoni baada ya kucheza mechi 25.


RAMADHAN Nswanzurimo, Kocha Mkuu wa Singida United amesema kuwa jana Februari 29 walipaswa waifunge Polisi Tanzania mabao 5-0 ila bahati haikuwa yao kutokana na wachezaji kushindwa kumalizia nafasi walizozipata.

Singida United ilipoteza mchezo wake kwa kufungwa bao 1-0 lililolofungwa na Sixtus Sabilo kwa mkwaju wa penalti huku mkwaju wa Singida United uliopigwa kutokana na mabeki kucheza faulo ndani ya 18 kupanguliwa na Manyika Jr.

Nswanzurimo amesem: "Siwezi kuingia ndani kucheza kwani tulipanga kumaliza mchezo mapema ndani ya kipindi cha kwanza mwisho wa siku ikawa ngumu.

"Tulipata nafasi za kufunga mabao matano na haijawa hivyo sina chaguo kwa kuwa matokeo yameshatokeo,".

Singida United inaendelea kuburuza mkia ikiwa imecheza mechi 25 ina pointi 12 kibindoni.


DITRAM Nchimbi, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa Kocha Mkuu Luc Eymael alimwambia kuwa akatumie makosa ya wapinzani ili akaifungie timu yake mabao.

Jana, Februari 29, Yanga ilishinda mbele ya Alliance mabao 2-0 na kuifanya ifikishe pointi 44 ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo.

Nchimbi amesema:"Mwalimu aliniambia kwamba ninapaswa nitazame mapungufu ya wenzangu na nikafunge ili kuipa timu ushindi na mwisho wa siku ndicho kilichotokea,".

Yanga imeipiga nje ndani Alliance kwani mchezo wa kwanza uliochezwa CCM Kirumba ilishinda kwa mabao 2-1 na jana imeshinda mabao 2-0.


ISMAILA Sarr alianza kupeleka maumivu kwa wababe Liverpool dakika ya 54 kabla ya kuongeza msumari mwingine dakika ya 60 na kuifanya Watford kuwa timu ya kwanza kuitungua mabao 3-0 Liverpool ndani ya Ligi Kuu England.

Msumari wa mwisho na wa tatu ulipachikwa kimiani na Troy Deeney dakika ya 72 na kuifanya Liverpool kupoteana.

Leo Liverpool imepoteza ikiwa ugenini baada ya kucheza mechi 27 bila kupoteza na ilitoa sare moja mbele ya Manchester United.

Watford imetibua rekodi ya Liverpool na kuifanya ipoteze mchezo wa kwanza Ila ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 79 na Watford ipo nafasi ya 17 na pointi 27 zote zimecheza mechi 28.

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kosa lao kubwa ilikuwa kuzifunga Simba na Yanga kwenye Kombe la Mapinduzi jambo lililowafanya wakamiwe na timu nyingine wanapocheza.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa timu nyingi zimeanza kuwapigia hesabu kali kwa kucheza nao kwa kukamia jambo linalowapa matokeo mabovu.

"Tuliposhinda Kombe la Mapnduzi kwa kuwafunga vigogo Simba na Yanga hapo ndipo matatizo yalipoanzia, timu nyingi zilianza kucheza nasi kwa kutukamia jambo lililofanya mechi zetu zote kuwa ngumu.

"Wachezaji nao walikuwa na kazi ya kufanya ila walishindwa kupata matokeo mazuri, ni mbaya kwetu na inaumiza ila tutapambana kurejea kwenye ubora wetu," amesema. 

Mtibwa Sugar ilitwaa taji la Mapinduzi kwa kuifunga Simba bao 1-0 kwenye fainali na ilitinga hatua ya fainali kwa kuinyoosha Yanga kwa mikwaju 3-2 ya penalti baada ya sare ya kufungana bao 1-1 ndani ya dakika 90.


UONGOZI wa Simba umesema kuwa umejipanga kuona unapata matokeo mbele ya KMC kwenye mchezo wa kesho utakaochezwa Uwanja wa Taifa majira ya saa 1:00.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandnbroeck amesema kuwa anatambua mchezo utakuwa mgumu ila anaamini watapata pointi tatu.

"Kila kitu ni hatua na kwa sasa ambapo tupo sio sehemu mbaya tunahitaji kuona tunapata matokeo mazuri yatakayotufanya tuzidi kuwa imara," amesema.

Simba inaongoza ligi ikiwa imecheza mechi 24 na ina pointi 62.

Uongozi wa Yanga umesema kuwa sababu kubwa ya muda wa mpira kubadilishwa mara kwa mara ni kutokana na timu ya Taifa ya Uganda kutaka kuutumia Uwanja wa Taifa kwa mazoezi.

Akizungumza na Saleh jembe, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga Atonio Nugaz amesema kuwa timu ya Uganda ya wanawake ilikuwa inahitaji kupata muda wa mazoezi.

"Timu ya Taifa ya Uganda ilikuwa inahitaji kupata muda wa kufanya mazoezi jambo ambalo lilichangia muda wa mpira kubadilika mara kwa mara," amesema.

Yanga itamenyana na Alliance Uwanja wa Taifa saa 1:00 jioni awali ulipangwa ucheze saa 10 na baadaye ulipelkwa mbele saa 11.


ABDALLAH Shaibu 'Ninja' ambaye ni beki na mshambuliaji kinda Nassor Mohamed aliyekuwa anakipiga Mtibwa B wamepata dili la kusepa kuelekea nchini Serbia kukipiga soka lao.

Ninja anakwenda timu ya RIGA FS nchini LATVIA na Nassor Saadun anakwenda nchini Serbia kuichezea OFK ZARKOVO.
Nyota hao wote wawili wamesajiliwa kwa kandarasi ya miaka miwili kuzitumikia timu hizo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ninja amesema kuwa mpango mkubwa ni kujituma ili kufikia malengo yake.


LIGI Kuu Tanzania Bara kuendelea leo kuchanja mbunga kwa timu 16 kuwa uwanjani kuzisaka pointi tatu muhimu.

Hizi hapa zitakutana leo, mechi zote zitapigwa saa 10:00 isipokuwa mechi ya Yanga na Alliance itapigwa saa 1:00 usiku.
Mwadui v Coastal Union , Kambarage

Singida v Polisi Tanzania, Namfua.

Kagera Sugar v Prisons, Kaitaba

Ruvu v Mbao, Mabatini
Biashara v Mbeya City, Karume.

Mtibwa v Ndanda, Gairo.

JKT Tanzania v Azam, Jamhuri

Yanga v Alliance, Taifa

FELIX Minziro, Kocha Mkuu wa Alliance amesema kuwa wanatambua wana kazi ngumu ya kufanya leo mbele ya Yanga ila wapo tayari hawana hofu.

Alliance itakaribishwa na Yanga Uwanja wa Taifa majira ya saa 11:00 jioni ikiwa ni mchezo wa pili kukutana msimu huu kwenye ligi.

Minziro amesema: "Tunawatambua wapinzani wetu hatuna hofu nao kwani wachezaji wapo sawa nasi tutapambana kupata pointi tatu muhimu,".

Mchezo wa kwanza Alliance ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.


ABDALAH Mohamed,'Bares', Kocha Mkuu wa JKT Tanzania amesema kuwa leo vijana wake watapambana mbele ya Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri.

Azam FC imeshatia timu mkoani Dodoma, leo itakuwa na kazi ya kumenyana na JKT Tanzania mchezo wake wa tatu ikiwa ugenini.

Bares amesema:"Kikosi kipo tayari na kila mchezaji amepewa majukumu yake ya kufanya, sapoti ya mashabiki inahitajika,".

Azam FC ilitoka kumalizana na Ndanda na Namungo, nyanda za juu kusini na iliambulia pointi moja na kupoteza nne kati ya sita baada ya kupata sare moja na Ndanda kisha ikachapwa na Namungo FC bao 1-0.


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga ndani ya mwezi Februari amekiongoza kikosi chake kucheza mechi saba za Ligi Kuu Bara.

Kwenye pointi 21 alizokuwa anasaka amejikusanya pointi 13 na kuziyeyusha pointi nane.

Hajapoteza mchezo hata mmoja ndani ya mwezi Februari, ameshuhudia jumla ya mabao sita wachezaji wake wakifunga huku akishuhudia wao wakiokota nyavuni mabao matatu.
  
Matokeo yake yapo namna hii:-Yanga 1-0 Mtibwa Sugar, Februari 2, Yanga 2-1 Lipuli, Februari 05, Ruvu Shooting 0-1 Yanga, Februari 08, Yanga 1-1 Mbeya City Februari 11, Yanga 0-0 Prisons, Februari 15, Polisi Tanzania 1-1 Yanga, Februari 18, Coastal Union 0-0 Yanga, Februari 23.


MWEZI Februari, mabingwa watetezi Simba wamecheza mechi saba za Ligi Kuu Bara na wameambulaia kichapo mechi moja mbele ya JKT Tanzania.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Uhuru, Februari 7 na bao pekee la ushindi lilifungwa na Adam Adam kwa kichwa mbee ya beki kisiki Pascal Wawa.

Simba ilikuwa inasaka pointi 21 imeambulia pointi 18 na tatu zimeyeyuka jumlajumla.

Kwa upande wa mabao ya kufunga, Simba imefunga mabao 12 huku ikikubali kufungwa mabaoa matatu.

Simba 2-0 Coastal Union, Februari 1, Simba 2-1 Polisi Tanzania, Simba 0-1 JKT Tanzania, Februari 7, Mtibwa Sugar 0-3 Simba, Februari 11, Lipuli 0-1 Simba , Februari 15, Simba 1-0 Kagera Sugar, Februari 18, Simba 3-1 Biashara United, Februari 22. 

John Bocco nahdha wao amekuwa kinara kwa mwezi Februari, ametupia mabao matatu na ametoa pasi moja ya  bao.


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umejipanga kusepa na pointi tatu leo mbele ya Alliance kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Taifa.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kikosi kipo tayari na wachezaji wana morali kubwa ya kusaka ushindi.

Bumbuli amesema:"Tumekuwa tukiambiwa wanyonge kutokana na matokeo ambayo tumekuwa tukiyapata hilo hatulijali kwa kuwa ubora wetu tunautambua na hatubahatishi tupo imara.

"Baada ya kumalizana na Gwambina sasa kazi inayofuata itakuwa dhidi ya Alliance, tupo tayari kuona tunapata ushindi kikubwa tunachotaji pointi tatu, mashabiki watupe sapoti,".

MABINGWA watetezi Simba kesho, Machi Mosi watakuwa Uwanja wa Taifa kumenyana na KMC mchezo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na kumbukumbu ya kushinda kwa mabao 2-0 Uwanja wa Uhuru kwenye mchezo wa kwanza msimu huu.
Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck imetoka kushinda mchezo wao wa Kombe la Shirikisho na kutinga hatua ya robo fainali, inakutana na KMC yenye hasira za kufungashiwa virago na Kagera Sugar kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.
Sven amesema kuwa amekiandaa kikosi chake kwa utulivu ili kuona kinashinda mbele ya KMC ili kupata pointi tatu muhimu.
“Tumetoka kushinda mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho mbele ya Stand United, macho yetu kwa sasa ni kwenye mchezo wetu wa ligi dhidi ya KMC, imani yangu tutapata matokeo chanya yatakayotupa pointi tatu” amesema.


ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa wamejipanga kuona wanapata ushindi mbele ya Ndanda FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Gairo.
Mwezi Februari, Mtibwa Sugar haijashinda mchezo kwenye mechi saba mfululizo ikiambulia pointi moja kati ya 21 ikiwa leo itafungwa itaacha jumla ya pointi 23 kwenye ligi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Katwila amesema kuwa watapambana kwenye mechi zinazofuata, matokeo yote yaliyopita haiwekezakani kuyabadilisha kwa kuwa yametokea.
“Ukishafungwa ama kupata sare hakuna unachoweza kukibadilisha zaidi ni kutazama namna gani timu ilifanya makosa na kuyarekebisha ili kuwa bora na kupata matokeo mazuri, mechi zetu nyingine tutapambana kupata matokeo,” amesema Katwila.
Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 24 imecheza mechi 24 itamenyana na Ndanda iliyo nafasi ya 14 na pointi zake 26.


IMEELEZWA kuwa nyota wa timu ya Yanga, Bernard Morrison ameongeza kandarasi ya mwaka mmoja na nusu ndani ya Klabu hiyo inayopambana kutwaa taji la Ligi Kuu Bara lililo mikononi mwa Simba.

Kiungo huyo mshambuliaji mwenye mabao mawili ndani ya Bongo na pasi tatu za mabao ilielezwa kuwa alikuwa kwenye hesabu za Simba ili wamtumie kwenye michuano ya kimataifa pamoja na timu nyingine mbili kutoka Afrika Kusini.

Habari zinaeleza kuwa mabosi wa Kampuni ya GSM wameamua kumalizana naye kwa kukaa naye chini na kumpa mkataba huo.

"Awali mkataba wake ulikuwa ni wa muda wa miezi sita ulikuwa unampa uhuru kuzungumza na timu nyingine na watani kama kawaida jicho lao limewashtua, ameongeza kandarasi ya mwaka mmoja na nusu.

"Kwa sasa presha imeshuka na kazi itafanyika bila mashaka kwani ana mkataba wa miaka miwili kwa sasa ndani ya Yanga," ilieleza taarifa hiyo.


Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 17 Bakari Shime amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kesho Uwanja wa Taifa kuipa sapoti timu hiyo itakapomenyana na Uganda.

Mchezo huo wa kesho utaanza saa 9 alasiri ni maalumu kwa ajiri ya kufuzu Kombe la Dunia linalotarajiwa kufanyika nchini India.

 "Wachezaji wapo sawa na kila kitu kinakwenda vizuri, kikubwa ni kwa mashabiki kujitokeza kuipa sapoti timu yao ya Taifa ili ifanye vema na kuanza kuisaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia," amesema.


LEO Februari 29 Yanga itawakaribisha Alliance kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.
Rekodi zinaonyesha kwamba Alliance iliyopanda Daraja msimu wa 2018/19 haijaambulia pointi mbele ya Yanga na ilianza kukutana na balaa Heritier Makambo na ocha Mkuu, Mwinyi Zahera.
Aliance iliyo chini ya Kocha Mkuu, Felix Minziro itakutana na Yanga inaliyoandamwa na matokeo ya sare kwenye mechi zake nne za ligi ilizocheza.
Kwenye mechi tatu ambazo wamekutana, Yanga imefunga mabao sita na imefungwa mabao mawili na Alliance, kwenye mchezo wao wa msimu huu Novemba 29 Yanga ilishinda mabao 2-1 hivyo leo Alliance watakuwa na kazi ya kulipa kisasi.
Matokeo yao yalikuwa namna hii:-Oktoba 2018 Uwanja wa Taifa, Yanga 3-0 Alliance, Machi 2, 2019 Alliance 0-1 Yanga Uwanja wa CCM Kirumba.

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.