Kikosi cha Simba kesho asubuhi kitasafiri kwenda Unguja, Zanzibar kwa ajili ya kambi ya pamoja kujiandaa na mchezo wao awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.


Yanga wanatarajiwa kucheza mchezo huo Jumapili hii dhidi ya Township Rollers kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten alisema kuwa wakiwa kambini huko watacheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Malindi na Mlandege.


Ten alisema kuwa timu hiyo itarejea Dar Ijumaa hii usiku na moja kwa moja wataingia kambini kwa ajili ya mchezo huo.



“Timu inakwenda kuweka kambi Zanzibar ni baada ya kupokea mapendekezo ya kocha wetu Zahera (Mwinyi) tukiwa huko tutacheza michezo miwili ya kirafiki kabla ya kurejea Dar kuwavaa Township Rollers,” alisema Ten.
Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.