MEDDIE Kagere mshambuliaji wa Simba, leo ameibuka shujaa kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Power Dynamo ya Zambia baada ya kupiga 'hat trick' wakati Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya mabingwa hao mara 7 kutoka Zambia.

Mchezo wa leo ambao ulikuwa ni hitimisho la kilele cha SportPesa Simba Wiki ulihudhuriwa na mashabiki wengi huku mgeni rasmi akiwa ni Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim ulikuwa na ushindani kutokana na kila timu kutafuta ushindi kwa hali na mali.

Kagere alianza kucheka na nyavu ndani ya Uwanja wa Taifa dakika ya 3 baada ya mlinda mlango wa Power Dynamo kujichanganya na kutoa pasi iliyomkuta Kagere ambaye hakufanya hiyana na akarejea tena kucheka na nyavu dakika ya 58 akimalizia pasi maridadi iliyopigwa na Deo Kanda kabla ya kukomelea msumari wa mwisho dakika ya 77.

Bao la kufutia machozi kwa Power Dynamo lilipatikana kipindi cha kwanza dakika ya 24 na liliwekwa kimiani na Jimmy baada ya mabeki wa Simba kujichanganya kuokoa kona iliyopigwa na wapinzani.

Kipindi cha pili Simba walichangamka na Miraj Athuman alikosa bao la wazi dakika ya 78 baada ya Mohamed Hussein 'Tshabalala' kuachia pasi sukari iliyoshindwa kujaa vizuri mguuni mwa Miraji na Clatous Chama naye dakika ya 80 alikosa bao la wazi baada ya kupigiwa pasi sukari na Meddie Kagere. 

Kagere amesepa na mpira wake leo baada ya kufunga 'hat trick' yake ya kwanza leo uwanja wa Taifa baada ya Ligi kuu kumalizika na inatarajiwa kuanza Agosti 23.
Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.