UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kwa sasa unafanyia kazi mapungufu ya kikosi hicho kwa ajili ya mchezo wa kimataifa dhidi ya Kenema ya Ethiopia.
Azam FC itamenyana na Kenema kwenye mchezo wa awali wa kombe la Shirikisho Agosti 10 na wanaendelea na maandalizi ya mwisho kwa sasa.
Idd Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC, amesema kuwa kazi kubwa iliyopo kwa sasa ni kusuka kikosi cha ushindani ambacho kitapata matokeo chanya kwenye mchezo wao wa kwanza.
"Kazi yetu kwa sasa ipo kwenye kutengeneza muunganiko mzuri wa kikosi bora kwa ajili ya mchezo wa kimataifa na tuna imani ya kufanya vizuri, kila kitu kitakuwa sawa.
"Ushindani upo nasi tumejipanga hasa kwa kufanyia kazi makosa madogomadogo ambayo yapo hasa kwenye safu ya ushambuliaji kwa sasa," amesema.
Post a Comment