APR inaamini kwamba ikimpata Kagere itakuwa na nafasi ya kupeta kwenye michuano ya kimataifa kutokana na uzoefu wa nyota huyo kwenye mechi kubwa na ngumu.
Kagere aliweza kutimiza majukumu yake vema msimu wake wa kwanza 2018/19 na timu yake ilitinga hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika jambo linalowafanya APR wazidi kuhaha kuipata saini yake.
"Mpango mkubwa wa APR inahitaji kupata saini ya Kagere na inahitaji pia kumboreshea zaidi mkataba wake ili iwe ngumu kumtoa akishasaini pale," ilieleza taarifa hiyo.
Eto Mupenzi, wakala anayewauzia wachezaji APR amesema kuwa:"Kuna mpango wa kuboresha thamani kwa wachezaji watakaotua ndani ya APR hivyo ishu ya Kagere bado sijajajua ipoje lada tusubiri," amesema
Post a Comment