UONGOZI wa Klabu ya Yanga chini ya Mwenyekiti Dk.Mshindo Msolla, umesema kuwa umeandaa jarida maalumu ambalo litakuwa na mambo mengi ambayo yanaihusu Yanga.
Jarida hilo linalohusu mambo mbalimbali ya klabu lilizinduliwa Aprili 30 limeambatana na neema kibao kwa mashabiki wa Yanga.
Jarida hilo lina kurasa 48 litakuwa likiuzwa kwa bei ya shilingi 5,000 nchini kote kupitia matawi mbalimbali ya Yanga.
Mwenyekiti Msolla amesema kuwa jarida hilo limetengenezwa kwa niaba ya mashabiki wa timu hiyo kwa ajili ya kulisoma ili kufahamu mambo mbalimbali yanayoihusu timu hiyo, na kwa ambao watanunua jezi za timu hiyo katika maduka ya GSM, watalipata jarida hilo bure.
“Jarida letu hili tumeliandaa kwa ajili ya kuwaelimisha mashabiki wetu mambo mbalimbali yaliyotokea zamani na sasa, ambapo jarida hili litapatikana kwa Sh 5000 tu ila kwa wale ambao watanunua jezi za Yanga katika maduka ya GSM watalipata jarida hili bure kabisa,” amesema.
Post a Comment