WACHEZAJI wa Real Madrid, wanatarajiwa kuanza mazoezi Mei 11, mwaka huu ambapo yatakuwa mazoezi binfasi.

Mazoezi hayo yatafanyika kwa uangalizi maalum huku yakiwa na wachezaji na makocha wachache.

Wachezaji mbalimbali wa La Liga, wiki ijayo wanatarajiwa kupimwa afya zao kuonekana kama hawana maambukizi ya corona.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni kuona kila mmoja anakuwa salama kuanzia wachezaji hadi makocha kabla ya kuanza mazoezi ya pamoja na kucheza michezo ya La Liga.

Kwa sasa wachezaji wote wa Real Madrid, wataendelea kufanya mazoezi binafsi hadi hapo Mei 11, ambapo watatakiwa kwenda kwenye viwanja vyao vya mazoezi vijulikanavyo kama Valdebebas

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.