JANGA la Virusi vya Corona limeacha balaa kubwa katika klabu mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Barcelonaambapo imepanga kuuza mastaa wake akiwemo Luis Suarez ili kujiingizia fedha.
Kutokana na La Liga kusimama hivi sasa huku ikitarajiwa kurudi kwa kuchezwa bila ya mashabiki, Barcelona inaangalia njia mbadala ya kupata vyanzo vya mapato ndiyo maana inataka kuuza mastaa wake.
Klabu mbalimbali zinazoshiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS), zinatajwa kumuwania kwa nguvu Suarez.
Mmiliki wa Klabu ya Inter Miami, David Beckham, amenukuliwa akisema kuwa, atafurahi kuona nyota huyo akitua kwao.
Hivi karibuni, Suarez alisema: "Huwezi jua, bado nina mkataba na Barcelona, lakini kwa mustakabali wa maisha ya baadaye, naona Ligi ya Marekani inavutia sana kwangu, ni sehemu nzuri."
Mkataba wa Suarez ndani ya Barcelona unaenda hadi 2021 ambapo kuna kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi chenye masharti ya kucheza mechi kwa asilimia 60 msimu ujao
Post a Comment