MSHINDO Msolla, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, amesema kuwa mambo mengi ya klabu hiyo yamesimamishwa kwa muda kutokana na janga la Virusi vya Corona.
Msolla amesema kuwa miongoni mwa michakato ambayo imesimamishwa ni pamoja na ule wa kwenda mfumo wa kimabadiliko, ujezi wa uwanja na mchakato wa kubadili katiba ya klabu.
“Kutokana na uwepo wa Ugonjwa wa Covid-19 ambao ni hatari kwa afya zetu, tumeona tusitishe michakato yote kuanzia ule wa ubadilishwaji wa klabu kimfumo wa uendeshwaji, uundwaji wa katiba mpya na ule mchakato wa ujenzi wa uwanja wetu kule Kigamboni.
"Ugonjwa huu ni hatari kwa afya zetu hivyo ni muhimu kila mmoja kuchukua tahadhari, kuhusu tutaanza lini ni mpaka pale kamati tendaji itakapotangaza tena,” amesema
Post a Comment