SVEN Yidah, kiungo anayekipiga Klabu ya Kariobang Sharks ya Kenya amesema yupo tayari kusaini ndani ya Yanga ili kucheza kwa mabingwa hao wa kihistoria kutokana na kukubali uwezo wao.
Kiungo huyo amekuwa akitajwa kutua Jangwani msimu ujao ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kilicho chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael raia wa Ubelgiji.
"Nimewahi kuzungumza na kiongozi mmoja wa Yanga ambaye anahusika na masuala ya usajili na alinieleza kuwa wanahitaji kupata huduma yangu jambo hilo kwangu naona ni jema kwani mchezaji kazi yake kucheza.
"Ninavutiwa na Klabu ya Yanga kwani niliwahi kukutana nao uwanjani wakati mmoja kwenye mechi yetu ile siku ya Wananchi, ninapenda kuwa mmoja wa wachezaji wao,' amesema
Post a Comment