STRAIKA wa Dortmund, Erling Haaland, amesema wala hajajisikia vibaya kuona nyota wa PSG, wanaiga staili yake ya kushangilia ambapo wengi waliitafsiri kama wanamkejeli.
Baadhi ya wachezaji wa PSG akiwemo Neymar na Kylian Mbappe, walionekana kushangilia kama Haaland katika Uwanja wa Parc des Princes ambapo PSG walishinda mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kusonga mbele.
Ikumbukwe kuwa, katika mchezo wa kwanza, Haaland alifunga bao na kushangilia ile staili yake ya kukaa chini na kukunja miguu, huku akinyoosha vidole juu. Staili hiyo ndiyo imeigwa na nyota hao wa PSG.
"Nadhani wamenisaidia kwa kiasi kikubwa katika kuitangaza staili yangu hii na kufika mbali zaidi, nawashukuru sana," alisema Haaland
Post a Comment