SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa miongoni mwa msosi anaopenda kula ni pamoja na samaki wale wa Bahari ya Hindi kwa kuwa wana ladha ya kipekee.
Sven ameongoza mechi 18 ndani ya Klabu ya Simba baada ya kupokea mikoba ya Patrick Aussems ambaye alipigwa chini baada ya kuongoza mechi 10 za ligi.
"Ninapenda kula samaki wale wa Bahari ya Hindi ni wazuri na watamu hivyo nimekuwa nikipenda kula mara nyingi baada ya kufika hapa Tanzania," amesema.
Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona ambalo linaitikisa dunia kwa sasa
Post a Comment