UONGOZI wa Azam FC umeionya Simba juu ya beki wao Yakub Mohamed ambaye anahusishwa kujiunga na mabingwa hao watetezi kwa kusema kuwa hawaruhusiwi kufanya naye mazungumzo kwa kuwa bado ana mkataba na Azam FC.

Imekuwa ikiripotiwa kuwa Simba ipo kwenye hesabu za kuipata saini ya beki huyo ili akaungane na Pascal Wawa, Erasto Nyoni kusongesha gurudumu ndani ya Simba.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdululkarim Amin, amesema kuwa ni kosa la kisheria kwa klabu yoyote kufanya mazungumzo na mchezaji wao Yakub kwani bado ana mkataba.

"Yakub ni mali ya Azam FC bado ana mkataba kwa sasa hivyo ni kosa kisheria kufanya naye mazungumzo ikibainika kwa klabu yoyote ile tutaichukulia hatua kwa kuwa ni makosa," amesema.

Tayari Azam FC imemuongezea kandarasi ya mwaka mmoja mshambuliaji wao namba moja Obrey Chirwa ambaye alikuwa anahusishwa kujiunga na Yanga

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.