MSHAMBULIAJI wa timu ya Kagera Sugar,Yusuf Mhilu amesema yupo tayari kukipiga Klabu ya Yanga
kama uongozi wa klabu hiyo utafuata utaratibu wa usajili.

Mhilu amesema kwamba kwa sasa bado hajafanya mazungumzo na Yanga zaidi ya kusikia tetesi kwamba anahitajika na klabu hiyo aliyowahi kuitumikia pia. 

"Nimekuwa nikiskia kwamba Yanga inahitaji huduma yangu hilo sio jambo baya kwani mchezaji thamani yake ni pale ambapo anakuwa anaonekana na timu nyingine, sina tatizo iwapo utaratibu utafuatwa mimi nitasaini bila hiyana," amesema.

Mhilu ametupia mabao 11 ndani ya Kagera Sugar akiwa ni miongoni mwa wazawa wenye urafiki na nyavu.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.