MAALIM Busungu, mshambuliaji wa zamani wa Yanga amesema kuwa kwa sasa ni muhimu kila mmoja akachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
Busungu amesema kuwa hali inaweza kuwa salama iwapo kila mmoja akachukua tahadhari dhidi Corona na kujilinda yeye kwanza na jamii kiujumla.
"Kwa kipindi hiki kigumu ambacho tunapitia ni muhimu kila mmoja akachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona kwani ni janga hatari ambalo linaitikisa dunia.
"Iwapo kila mmoja akachukua tahadhari itakuwa rahisi kwake kujilinda na kuwalinda wengine, yale maelekezo yanayotolewa na Wizara ya afya pamoja na Serikali yasipuuzwe," amesema.
Post a Comment