BAADA ya PSG kutangazwa kuwa ni mabingwa wa Ligi Kuu Ufaransa ‘Ligue 1’, beki na nahodha wa timu hiyo, Thiago Silva, ameugawa ubingwa huo kwa madaktari dunia nzima.
Hivi karibuni, PSG walitangazwa kuwa mabingwa wa Ligue 1, baada ya kufahamika kuwa ligi hiyo haiwezi kuendelea tena kwa msimu huu.
Kutokana na madhara ya virusi vya Corona ambavyo vimevamia dunia nzima kwa sasa, Ufaransa wao wametangaza kuwa ligi hiyo imefutwa kwa kuwa serikali ya nchi hiyo imesema kuwa michezo itaruhusiwa kuendelea tena, Septemba mwaka huu.
Silva amesema ubingwa huo ni kwa ajili ya madaktari wote ambao wanapambana na virusi vya Corona duniani kote kwa kuwa wanafanya kazi ngumu sana na hatari.
Wakati ligi hiyo inasimama Machi, mwaka huu kabla ya msimu kuahirishwa kabisa, PSG walikuwa mbele kileleni kwa tofauti ya pointi 12 na mchezo mmoja mkononi.
“Huu ubingwa unabaki kuwa alama tosha kwenye mafanikio yetu.
“Ninachoweza ni kumshukuru Mungu kwa kutwaa ubingwa wa saba katika miaka nane niliyokaa Ligue 1.
“Hakika nisingeweza kufika hapa kama siyo sapoti ya familia, lakini hakika ubingwa huu ni maalum kwa ajili ya madaktari wote duniani ambao wanapambana na virusi vya Corona,” aliandika beki huyo raia wa Brazil katika akaunti yake ya Instagram.
Post a Comment