PAPY Tshishimbi, kiungo wa Yanga amesema kuwa yupo tayari kupiga kazi na nyota yeyote atakayesajiliwa ndani ya kikosi hicho.
Miongoni mwa nyota wanaotajwa kutua ndani ya Yanga msimu ujao ni pamoja na Yidah Sven anayekipiga Kariobargs Sharks ya nchini Kenya ambaye ni kiungo.
Tshishimbi amesema:"Siku zote lazima ukubali ushindani na changamoto hivyo ninaamini namna ambavyo kutakuwa na ushindani ndivyo ambavyo nami pia nitakuwa bora.
"Ninataka kucheza katika kikosi cha kwanza na ni malengo ya wachezaji wengi ili kuendeleza uwezo wao sasa ili kuwa kikosi cha kwanza ni lazima upambane uwe bora, kwa wale ambao watakuja ni jambo jema" amesema.
Ndani ya Yanga, Tshishimbi anavaa kitambaa cha unahodha, kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona alikuwa ametoa pasi moja ya bao kati ya mabao 31 yaliyofungwa na Yanga
Post a Comment