DIKSON Job, beki chipukizi wa Mtibwa Sugar ameziingiza vitani klabu mbili ambazo ni Simba na Yanga zinazohaha kupata saini yake.
Simba inaelezwa kuwa ilianza kumfuatilia nyota huyo kitambo ila ghafla Yanga nao wameibuka baada ya beki kisiki Kelvin Yondani kuelezwa kuwa kumtaja Job kuwa mbadala wake.
Habari kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa Yondani amewashauri mabosi hao kumvuta ndani ya kikosi Job ambaye anauwezo mkubwa licha ya kuwa chipukizi.
"Yanga imehamisha nguvu kwa beki Job ili kupata saini yake huo ni ushauri wa beki kisiki Yondani ambaye ana ushawishi mkubwa kwa wachezaji wengi ambao wanajifunza mengi kwake," ilieleza taarifa hiyo.
Hassan Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa taarifa hizo sio rasmi kwa kuwa hazijafika mezani kwake
Post a Comment