KUNA hatihati kwa Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga, kutoendelea kama ilivyokuwa imepangwa kutokana na wachezaji watatu wa timu ya Cologne kukutwa na virusi vya Corona.
Timu nyingi za Ujerumani zilikuwa zimeanza mazoezi, lakini juzi wakati wachezaji wakipimwa kabla ya kuanza mazoezi watatu kati yao walikuwa na virusi vya Corona.
Ligi hiyo ilikuwa imesimama kuanzia mwezi Machi na sasa timu zilikuwa zimeanza mazoezi na ikawa inaonekana kuwa hali imeanza kuwa mbaya.
Hata hivyo, utaratibu wa mazoezi ni kwamba kabla ya kuanza kila mchezaji anatakiwa kupiwa kama ana virusi hivyo au la.
Hata hivyo, pamoja na kwamba Ujerumani hawatoa taarifa yoyote, lakini timu hiyo ya Cologne yenyewe imesema kuwa bado itaendelea na mazoezi bila hao wachezaji watatu.
Hata hivyo, taarifa yao ilisema kuwa hawaruhusiwi kuwataja majina wachezaji hao ambao wana virusi hivyo.
Ligi hiyo ambayo mwanzoni ilitagazwa kuwa ingeendelea Mei 9, sasa tarehe imebadilishwa hadi Mei 16 kwa usalama zaidi.
Post a Comment