UONGOZI wa Simba umesema kuwa Rais John Magufuli anaonyesha nini maana ya uongozi baada ya leo kusema kuwa anafikiria kurejesha lizi zote za Bongo.

Magufuli amesema:"Nafikiria kurejesha ligi ili ziendelee kwa kuwa hakuna mchezaji ambaye amepata madhara makubwa dhidi ya Corona hivyo kutowaruhusu wacheze tutakuwa tunataka wapate Corona.

Baada ya kauli hiyo ya JPM, Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema:-"Thanks Mr President,( Asante Rais) ligi inaweza kuchezwa bila watazamaji na bingwa halali kupatikana na ikiwapendeza inaweza kuchezwa katika kituo kimoja. Timu zote zikaja Dar, kama itakuwa ni ngumu kusafiri kila siku.

"Kwa mara nyingine Rais wangu unaonyesha uongozi ni nini," .


Machi 17 Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ilisimamisha ligi zote baada ya kupatikana mgonjwa wa kwanza mwenye Virusi vya Corona

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.