UONGOZI wa Azam FC umefunguka kuwa kutokana na uwepo wa maambukizi ya Virusi vya Corona kumesababisha majembe ya maana kushindwa kutua klabuni hapo.
Mabosi hao wameongeza kwamba virusi hivyo vimetibua mambo kwani kuna baadhi ya wachezaji ambao walikuwa wanawahitaji nchi zao kwa sasa zimewekwa ‘lockdown’ kusababisha mazungumzo kushindwa kufanyika vizuri.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema kwamba tayari wana majina ya wachezaji hao kwenye orodha yao lakini wanashindwa kukamilisha suala la kuwasajili kwa sababu timu zao kwa sasa hazifanyi lolote kwa sababu ya ugonjwa huo.
“Tuna majina ya wachezaji kadhaa ambao tunawahitaji hasa wale wa kimataifa lakini mambo yanakuwa magumu kwa sababu wako lockdown.
“Kwa sababu hiyo yanachukua muda kidogo kwani klabu za nje zenyewe ndiyo ziko kwenye hali hiyo,” alisema Popat
Post a Comment