RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli amesema kuwa anafikiria kurejesha ligi zote Bongo.

Machi 17, Ligi Kuu Tanzania Bara ilisimamishwa na Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Magufuli amesema:"Watanzania tusiwe na hofu, tuendelee kuchapa kazi, wanasiasa waache kutumia hii kama ajenda, haitaweza kuwasaidia, Watanzania lazima tuishi, kwa siku zinazoendelea ninafikiri kuruhusu hata ligi za mipira ziendelee, nasubiri wataalamu wangu wanishauri," .

Ligi zote ikiwa ni Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili,Ligi za Wanawake kwa sasa zimesimama

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.