UONGOZI wa Yanga umesema kuwa njia bora ya kumpata bingwa wa Ligi Kuu Bara ni mpira kuchezwa uwanjani ikishindikana basi matokeo yote yafutwe ili kuanza upya.
Kwa sasa ligi imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia nzima ambapo wakati inasimishwa Yanga ilikuwa nafasi ya tatu na pointi zake 51.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa:-"Njia bora ya kumpata bingwa ni uwanjani ambapo mechi zikichezwa inakuwa rahisi kumpata bingwa kwani kwa sasa kinara akipewa kombe atakuwa anatuonea sisi pia tuna nafasi ya kuwa mabingwa.
"Tuna mechi za viporo hatujacheza na kikosi kilikuwa kinachanganya, majirani zetu Kenya hata ukiangalia Angola walikuwa wana kanuni za dharula lakini sisi hilo halipo hivyo itapendeza bingwa atafutwe uwanjani ama msimu ufutwe kusiwe na bingwa," amesema.
Kinara wa ligi ni Simba ana pointi 71 kibindoni baada ya kucheza mechi 28
Post a Comment