KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amesema kuwa kazi pekee iliyomleta nchini ni kuhakikisha anaifanikisha Yanga kupata mabao jambo linalomfanya aukumbuke uwanja wa mpira.
Raia huyo wa Ghana ni ingizo jipya ambaye alijiunga na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili ikiwa ni pendekezo la Kocha Mkuu, Lucy Eymael.
Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa na Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona.
Morrison amesema:-"Kikubwa ambacho kilinileta Yanga ni kutimiza kazi yangu ambayo ni kufunga mabao ama kutengeneza nafasi ya kufunga hivyo kwa sasa kuna mengi ninayakumbuka ikiwa ni pamoja na uwanja.
"Ombi langu ni kuona kwamba kila kitu kinakuwa sawa na ligi inaweza kurejea jambo ambalo litanifanya niwe na furaha katika kutimiza majukumu yangu," .
Morrison amecheza mechi 10 za ligi akitupia mabao matatu na kutengeneza nafasi tatu za kufunga kati ya mabao 31 ya Yanga.
Post a Comment