KLABU ya Alliance FC yenye maskani yake Mwanza haikuwa na kasi nzuri msimu huu kabla ya ligi kusimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vyua Corona.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi 29 ilijikusanyia pointi 29 ina wastani wa kukusanya pointi moja kila mchezo ndani ya ligi.
Kwenye mmsimamo ipo nafasi ya 18 baada ya kuzimega dakika 2,610.
Imetupia jumla ya mabao 23 kibindoni huku ikibebeshwa jumla ya mabao 36.
Ina wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 113 huku ikiwa na wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 72.
Post a Comment