JUMA Nyosso, nahodha wa timu ya Kagera Sugar amesema kuwa ni muhimu kwa kila mmoja kwa sasa kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia.

Nyosso amesema:-'Wakati huu ni muhimu kila mmoja akachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona ili kujilinda yeye na jamii kiujumla," .

Kagera Sugar iliyo chini ya Kocha Mkuu Mecky Maxime ni miongoni mwa timu zilizokuwa zinaleta ushindani msimu huu.

Ipo nafasi ya 8 ikiwa na pointi 41 kibindoni baada ya kucheza mechi 29 za ligi na imefungwa mabao 31 huku ikifunga 36.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.