DUNIA nzima kwa sasa ipo kwenye vita dhidi ya Virusi vya Corona ambavyo vimesababisha mipango mingi kusimama kwa muda kwa sasa hilo lipo wazi.
Kila mmoja analia kwa wakati wake kwa namna ambavyo anapata muda kufanya dua zake kwa Mungu wake hilo ni jambo la msingi pia kwa sasa.
Tumeona kwamba wapo wale ambao wameanza kujitoa wao wenyewe binafsi kwa ajili ya kutoa misaada kwa jamii ili kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya Corona.
Katika hili ninawapa pongezi kwani wamechagua fugu jema ambalo lina Baraka kutoka kwa Mungu na ndivyo ambavyo inapaswa iwe siku zote kila siku katika vita.
Ni wakati mmoja ambao maadui huzungumza lugha moja kwa wakati mmoja lengo likiwa kutafuta ushindi kwani iwapo ule uadui utaendelea inakuwa rahisi kuangamia.
Ninapenda kuona kwamba kwa sasa hakuna makundi ambayo hayana maana hilo lipo wazi kwani ukianza kwa mashabiki si wale wa Mtibwa Sugar, Kagera Sugar hata zile klabu za Kariakoo Simba na Yanga wote kwa sasa wapo vitani.
Lugha zao zimekuwa zinaeleweka hakuna ambaye anazungumza kuhusu faulo ya Jaffary Kibaya wala namna Bigirimana Blaise alivyokosa bao akiwa ndani ya 18 hilo halipo kwa sasa.
Wimbo umekuwa ni mmoja tu namna ya kupambana na Virusi vya Corona hilo ni muhimu kuliendeleza usiku hata mchana mpaka pale vita itakapoisha.
Kuna jambo ambalo bado naona limekuwa kimya kwa sasa kwa timu zetu kuwa mstari wa mbele katika kupambana na Corona kwa vitendo.
Tunaona kwamba kwa sasa wameachiwa wachezaji wenyewe wafanye kwa kujitegemea wao wenyewe bila kuwa na ile sapoti ya timu zao.
Ibrahim Ajibu wa Simba amekuwa na mradi wake ambapo anawatembelea watoto yatima na kutoa misaada kwa kadri ambavyo ameguswa katika hilo anastahili pongezi.
Kwa timu pia nimeona Pamba SC ile inayoshiriki Lgi Daraja la Kwanza ikifungua njia yake kwa kujitoa kwa kuwatembelea wenye uhitaji na kutoa pale ambapo wamefanikiwa kupata.
Zote ni jitihada za baadhi ya wale ambao wanapambana kuendeleza vita dhidi ya Virusi vya Corona, wapo wapi wale waliokuwa na nguvu ya kumwaga fedha kwa wachezaji baada ya mechi kuisha?
Wakati sahihi wa kujitokeza na kupambana kwa vitendo ni sasa tukishinda vita hii ndipo tutakuwa ni mashujaa na tutarejea kumwaga zile pesa kwa wakati mwingine kwa kuwa adui yetu tumemshinda.
Naona klabu zinapambana kutoa elimu kwenye mitandao ya kijamii na kuendelea kufanya yale yanayostahili ndio ni jambo jema ila muda wa kuwa kwenye istagram kwa sasa umekwisha.
Ni wakati wa timu zote kuungana na kuwa na nguvu moja kwa kujitoa katika kupambana na Virusi vya Corona kwa nguvu moja.
Ninaamini iwapo timu zote zitaungana na kufanya yale wanayoyafikira kwa vitendo itakuwa rahisi kumshinda adui ambaye anatufanya tukose ule uhondo wa ligi.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.