KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Etienne Ndayiragije amesema miongoni mwa vitu anavyovitazama kabla ya kumpa mchezaji kitambaa cha unahodha ni uwezo wake wa kuongoza pamoja na nidhamu.
Ndayiragije amesema anaamini katika mawazo ya kila mmoja jambo linalomfanya awe na maelewano na wachezaji.
"Mimi napenda sana kumteua mchezaji ambaye ataweza kunikumbusha na kunipa ushauri, uwezo wake wa kujituma na kuongoza ni mambo ya msingi bila kusahau nidhamu binafsi," amesema.
Stars ilivunja kambi ya maandalizi dhidi ya Chan kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
Post a Comment