KIKOSI cha Coastal Union ni miongoni mwa timu yenye ushindani mkubwa na wachezaji makini ambao inaelezwa kuwa uwezo wao umewaweka sokoni.
Wachezaji wake saba wa kikosi cha kwanza iwapo mambo yatakuwa sawa basi nafasi za kusepa kwao ni kubwa ndani ya kikosi cha Wagosi wa Kaya.
Hawa hapa wanatajkwa kutazamwa kwa ukaribu kwa sasa:-
Bakar Mwamnyeto nahodha na beki wa kati anatajwa kuwa anawindwa na Simba na Yanga.
Ayoub Lyanga, mshambuliaji huyu anayajwa kuwindwa na Yanga.
Hassan Kibailo, beki huyu wa kulia anatajwa kuwindwa na Azam FC na Lipuli.
Shaban Dudu, mshambuliaji huyu anatajwa kuwindwa na Kagera Sugar, Namungo na Yanga.
James Kahimba, winga huyu anatajwa kuwindwa na Namungo, Polisi Tanzania.
Ame Ibrahim, beki huyu anatajwa kuwindwa na Simba, Yanga, Azam FC.
Hance Masoud, beki huyu anatajwa kuwindwa na Ruvu Shooting, Mwadui na JKT Tanzania.
Mitambo hii ya kazi inampa jeuri Mgunda kufanya vema uwanjani ambapo kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona, timu yake ilikuwa katika kasi.
Ipo nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa na pointi 46 kibindoni baada ya kucheza mechi 28
Post a Comment