UONGOZI wa Simba umesma kuwa hauna mashaka iwapo Ligi Kuu Tanzania Bara itafutwa kwani wanaamini haki yao ya kuwa was kimataifa itabaki kwao na sio kwenda Yanga ama Coastal Union.
Kwa sasa kumekuwa na hofu kubwa ya kuhusu hatma ya Ligi Kuu Bara kutokana na mlipuko wa Virusi nvya Corona ambao umesababisha ligi mbalimbali kufutwa ikiwa ni pamoja na ile ya Kenya ambapo mabingwa ni Gor Mahia.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema:"Kama Ligi Kuu Bara ikifutwa hatuna shida sisi kama Simba kwa sababu kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa tunajua hiyo ni nafasi yetu na siyo timu nyingine.
"Kwa sababu Ligi ikifutwa bado Simba atakuwa kileleni, ikiendelea Simba watakuwa Mabingwa hilo halina mjadala ni timu yetu kimataifa sio Yanga ama Coastal Union.
"Hao Fifa wakisema Ligi zao zifutwe lazima watayataka mashirikisho kuchagua wawakilishi wao wa mashindano ya kimataifa na kigezo kitakuwa kuchukua timu mbili zinazoongoza msimamo kwa hiyo hao wanaoshangilia inabidi wawe wapole," amesema.
Simba ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na poiti 71 baada ya kucheza mechi 28
Post a Comment