PAPY Kambamba Tshishimbi, nahodha wa Yanga amesema kuwa ni muhimu kila mmoja kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia kwa sasa.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia.
Tshishimbi amesema:"Ni ngumu kuendelea na mechi kwa sasa kutokana na janga la Virusi vya Corona ambavyo vipo hivyo ni vizuri kila mmoja kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
"Imani yangu ni kwamba iwapo kila mmoja atachukua tahadhari itatufanya tuwe salama na hata ligi ikirudi tuwe pamoja, kwa sasa ninaendelea na mazoezi ili kulinda kipaji changu," amesema.
Wakati ligi inasimama Yanga ilikuwa nafasi ya tatu ikiwa na pointi 51 kibindoni baada ya kucheza mechi 27
Post a Comment