SADIO Mane, nyota wa Senegal anayekipiga ndani ya Liverpool anazidi kuivuruga timu yake kutokana na mabosi wa Real Madrid kuendelea kusisitiza kuwa wanahitaji saini yake.

Mane mwenye miaka 28 amekuwa kwenye ubora wake msimu huu jambo linalofanya timu nyingi kuhitaji kupata saini yake.

Akiwa amejiunga mwaka 2016 Liverpool akitokea Southampton amecheza mechi 118 akiwa ametupia mabao 59 .


Pia Mane amekuwa bora ndani ya timu yake ya Taifa ya Senegal akiwa amecheza mechi 69 ametupia jumla ya mabao 19.

Jurgen Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool bado anaamini kuwa nyota huyo anastahili kubaki ndani ya kikosi chake ambacho kinaongoza Ligi Kuu England kikiwa na pointi 82 baada ya kucheza mechi 29

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.