LIONEL Messi, mshambuliaji namba moja ndani ya Barcelona bado anaushawishi uongozi wa klabu yake uipate saini ya Neymar Jr.
Inaelezwa kuwa Messi amemchagua Neymar badala ya Lautaro Martinez anayekipiga Inter Milan ambaye inaelezwa kuwa Barcelona wanaisaka saini yake.
Messi na Neymar Jr walikuwa ni washkaji wa muda mrefu wakati ule wa msimu wa 2013/17 walipokuwa pamoja Nou Camp.
Messi ndani ya La Liga ametupia mabao 19 timu yake ikiwa ni namba moja na ina pointi 58 kibindoni ikiwa imecheza mechi 27.
Post a Comment