MOHAMED Salah, raia wa Misri, nyota wa Liverpool amecheza mechi 100 ndani ya Liverpool tangu ajiunge nayo mwaka 2017 akitokea Klabu ya Roma ametupia jumla ya mabao 70.
Salah pia aliwahi kucheza ndani ya Chelsea ambapo hakuweza kuwika sana alipitia msoto mkali ilikuwa msimu wa 2014/15 ambapo alicheza mechi 13 na kutupia mabao mawili.
Jambo hilo liliwafanya mabosi wa Chelsea kumtoa kwa mkopo kwenda Fiorentina ambako alicheza mechi 16 na kufunga mabao sita akatolewa tena kwa mkopo kwenda Roma.
Huko alipewa dili la moja kwa moja baada ya msimu wa 2015/16 kucheza mechi 34 na kutupia mabao 14 dili lake lilipojibu alicheza mechi 31 ndani ya Roma msimu wa 2016/17 na kutupia mabao 15 ndipo akaibukia Liverpool.
Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp anaamini kuwa Salah atazidi kuwa bora iwapo ataongeza juhudi zaidi
Post a Comment