SHOMARI Kapombe, beki wa Simba ni miongoni mwa wachezaji anaowakubali Kocha Mkuu wa Namungo, Hitimana Thiery raia wa Burundi.
Kapombe amekuwa kwenye ubora wake msimu huu wa 2019/20 ndani ya Simba ambao ni vinara wakiwa na pointi 71 kibindoni.
Amehusika kwenye mabao matano kati ya 63 yaliyofungwa na Simba ambapo kazi yake ilikuwa ni kumwaga maji kutoka pembeni ya uwanja na guu lake la kulia ndilo lenye nguvu nyingi.
"Kwa nafasi yake yupo vizuri anajua kulinda na kuanzisha mashambulizi pia ni aina ya mabeki wanaojituma muda wote," amesema.
Post a Comment