PIERRE Emerick Aubameyang, mshambuliaji wa Arsenal alijiunga na washika bunduki hao msimu wa 2018 akitokea Klabu ya Borussia Dortmund.

Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Gabon na Arseanl pia amekuwa na balaa uwanjani amecheza jumla ya mechi 97 kwenye mashindano yote, kacheka na nyavu mara 61 ndani ya Arsenal.

Kumekuwa na presha kubwa kwa Arsenal juu ya kubaki na nyota huyo ambaye amesema kuwa anasubiri kuona nini kitatokea kwake kuhusu Arsenal.

Inatajwa kuwa Manchester United na Barcelona zinahitaji huduma za Auba ili akaonyeshe makeke yake  ya Wakada.

Mabosi zake Arsenal inaelezwa pia hawana hiyana iwapo kutakuwa na ofa nzuri wanaweza kufanya biashara. 

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.