JUMA Kaseja, nahodha wa KMC amesema kuwa kwa sasa anachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona huku akifanya mazoezi kulinda kipaji chake.

Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia kwa sasa.

Kaseja amesema:- "Nipo salama ninaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona pia ninafanya mazoezi binfsi ili kulinda kipaji changu.

"Kikubwa kwa sasa kila mmoja kuchukua tahadhari na kujilinda dhidi ya Virusi hivi kwani ni janga la dunia,". 

KMC ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo ikiwa na pointi 33 baada ya kucheza mechi 29.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.