IDD Seleman, 'Naldo' mshambuliaji wa Azam FC amesema kuwa miongoni mwa mechi ambayo ilikuwa na presha msimu huu ni ile dhidi ya Simba walipokubali kichapo cha mabao 3-2.
Azam FC iliyo chini ya Arstica Cioaba imepigwa nje ndani na Simba msimu wa 2019/20 ambapo mchezo wa kwanza ilikubali kichapo cha bao 1-0 na ule wa pili walichapwa mabao 3-2.
"Ulikuwa ni mchezo mgumu na presha kubwa ukizingatia kwamba tulianza kufunga tukaamini kwamba tutasepa na pointi tatu mambo yakawa tofauti," .
Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara imejikusanyia pointi 54 baada ya kucheza mechi 28.
Post a Comment