INAELEZWA kuwa mpango namba moja wa mabosi wa Simba ni kusuka kikosi bora ambacho kitafanya vema msimu ujao kwenye mechi za kitaifa na kimataifa.
Kwa sasa Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara ipo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji ambaye ameshataja majina ya wachezaji anaowakubali huku akianza na Lukas Kikoti anayekipiga ndani ya Namungo.
Wengine ambao inatajwa kuwa wapo kwenye rada za Simba ni pamoja na Justin Shonga nyota wa Orlando Pirates, Joash Onyango, beki wa kati wa timu ya Taifa ya Kenya, Bakari Mwamnyeto beki wa Coastal Union, Iddy Mobby, Baraka Majogoro, Sixtus Sabilo hawa wapo ndani ya Polisi Tanzania.
Lukas Kikoti na Relliants Lusajo wa Namungo ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa kwenye rada za Simba.
Sven amesema kuwa anahitaji kuwa na wachezaji mbadala zaidi ya wiwili kwenye kikosi chake.
Ligi ikiwa imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona, Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28.
Post a Comment